Mwigulu: Aliyemtisha Nape Kwa Bastola Sio Askari Polisi, Uchunguzi Sakata la Beni Saa Nane Bado Unaendelea
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema aliyemtishia bastola aliyekuwa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, hakuwa askari.
Amesema kijana hiyo alikuwa ni mhalifu aliyetumia nafasi ya mkutano wa Nape na waandishi habari kutaka kutekeleza tukio hilo ambapo aliishia kumtishia bastola.
“Awali tulidhani yule kijana ni polisi lakini hakuwa na sare za polisi, cha kwanza nilimuelekea Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kufuatilia na akaleta majibu kuwa hakuwa polisi,” amesema Mwigulu akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds leo.
Aidha, amesema suala la aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti nwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Ben Sanane ni ngumu kulisemea kwamba amefariki au yuko kwani polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
“Kwa aina ya taarifa ninazopata ni kama inaelekea kufikia ukomo ni jambo ambalo tumelipa uzito kulifanyia kazi na Mtanzania yeyote mwenye nia njema anaweza kutusaidia kufuatilia,” amesema.
No comments:
Post a Comment