Rais wa Zanzibar ateua viongozi wapya na kufanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi wapya na kufanya mabadiliko katika baadhi ya taasisi mbalimbali za Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema Dk Idris Muslim Hija ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Joseph Abdalla Meza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.
Wengine walioteuliwa ni Juma Ali Juma amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko, Bakari Haji Bakari amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar na Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko.
Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango, Kapteni Khatib Khamisi Mwidini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Unguja na Abeid Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, Pemba.
Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba na Salma Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni,Pemba.
Uteuzi huo umeanza Septemba 22, hivyo viongozi hao wanatakiwa kuripoti Ikulu Septemba 24 mwaka huu saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.
No comments:
Post a Comment