Naibu Waziri afunga Machimbo Mkuranga Pwani
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amefunga machimbo ya mchanga katika kijiji cha Kolangwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri Mpina amefikia uamuzi huo kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wachimbaji wa mchanga katika machimbo hayo.
Mpina ametoa agizo la kufungwa kwa machimbo hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Pwani ambapo amebaini uharibifu huo umechangiwa na Taasisi za Serikali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Idara ya Madini na Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Waziri amebaini kuwa uchimbaji huo umefanyika bila wananchi kushirikishwa na haukuzingatia miundombinu na sheria ya Mazingira pia makazi ya watu.
Kufuatia mapungufu hayo, Mpina ameagiza Taasisi hizo za Serikali kufuatilia uharibifu huo uliofanywa kwa muda wa wiki mbili.
No comments:
Post a Comment