MAJONZI: Watoto Waliotekwa Wakutwa Wamekufa Chooni

MAJONZI: Watoto Waliotekwa Wakutwa Wamekufa Chooni

Watoto 2 Ikram na Maureen, kati 4 waliotekwa wamepatikana wakiwa wamefariki dunia katika shimo la choo ambacho  bado halijaanza kutumika.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian huko Olasiti jijini Arusha, Daudi Safari, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi limeopoa miili ya watoto hao  jana jioni.

Inadaiwa kuwa mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya kuondoka na kuelekea Geita ambapo amekamatwa na kusema walipo watoto hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha taarifa za kukamatwa kwa mtekaji huyo aliyetambuliwa kwa jina la Samson Petro mwenye umri wa miaka 18.

Kamanda Mwabulambo amesema kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo mwenye miaka miwili.

Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha nyumba hiyo ya kulala wageni wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Ombeni Mshana na Elizabeth Ombeni.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages