Polisi yatoa ufafanuzi Vifo vya Watoto Watatu Waliofariki kwa Bomu Arusha

Polisi yatoa ufafanuzi Vifo vya Watoto Watatu Waliofariki kwa Bomu Arusha

Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitu wasivyovijua hasa vyenye asili ya chuma ili kuepusha madhara.

Kamanda Mkumbo ametoa hadhari hiyo alipokuwa akizungumzia tukio la vifo vya watoto watatu wakazi wa kata ya Loksale wilayani Monduli vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu walilookota wakati wanachunga mifugo na kuanza kulichezea kama mpira ambalo lililipuka na kuwajeruhi vibaya miguuni.

Akizungumza kwa njia ya simu kamanda Mkumbo amesema licha ya kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya lakini lingeweza kuepukika kama watoto hao wangeweza kutoa taarifa ya kitu walichokiona.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa watoto hao  wangeweza kufanya hivyo kama wangekuwa wanakumbushwa na wazazi wao mara kwa mara wanapokwenda machungani.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw. Iddy Kimanta aliyezungumza na ITV kwa njia ya Simu amesema watoto hao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi Nafko na wawili akiwemo Landisi Setabau miaka 12 na Samweli Nyandusi miaka 9 walikuwa wanasoma darasa la kwanza wakati mwingine aliyetajwa kwa jina la Seuri Losila miaka alikuwa darasa la tatu.

Viongozi wa eneo lililopotokea tukio hilo wamesema kimsingi tukio hilo ni bahati mbaya kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakielimishwa juu ya kufuata maelekezo na mara nyingi wamekuwa wakitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja kutoa taarifa wanapoona mabaki ya vyuma.

Kwa mujibu wa viongozi hao katika maeneo mengi ya wafugaji wakati wa likizo watoto huwasaidia wazazi wao kuchunga mifugo na pia wakati wote wamekuwa wakitoa taarifa wanapokutana na vitu kama hivyo na wahusika wamekuwa wakifika mara moja na kuvichukua.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages