Jaji Mku: Hatupo Tayari Kuzungumza Lolote Kuhusu Tundu Lissu
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema shambulio alilofanyiwa Tundu Lissu ni uhalifu mkubwa lakini majaji hawawezi kuzungumza juu ya tukio hilo kwani kanuni haziwaruhusu kutoa maoni au kuzungumzia jambo ambalo wanaona litakwenda mahakamani
Jaji Mkuu amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam na kusema amekuwa akiona watu wakitaka kusikia maoni yao juu ya tukio hilo na kuendelea kusema hawawezi kutoa maoni yao juu ya sakata hilo la Tundu Lissu kwa sababu wao mahakamani wana kanuni ambazo zinawazuia kutoa maoni au kuongelea jambo ambalo wanaona litakwenda mahakamani.
"Kwenye mitandao mmekuwa mkijaribu kutuvuta tutoe maoni sisi hatutasema kitu, tuache sheria zifanye kazi yake ila pale tutakapoona kwamba waliopewa jukumu la kukusanya ushahidi wanashindwa kufanya hivyo ndiyo tupige kelele. Kitu cha kwanza ni kukusanya ushahidi na huo ushahidi utakusanywa hapa hapa Tanzania asikudanganye mtu kwamba mtu kutoka nje ndiyo atakuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi hapa nyumbani bali ushahidi unakusanywa hapa hapa" alisema Jaji Mkuu wa Tanzania
Mbali na hilo Jaji Mkuu wa Tanzania amesema siku za karibuni kuna moja ya hakimu alishambuliwa na kuuwawa lakini wao kama majaji hawakuwahi kulalamika, au kusema jambo lolote, au kulaani jambo hilo wala kuwataka watu walaani kitendo hicho kwa kuwa kanuni zao haziwaruhusu kufanya hivyo.
Jaji Mkuu alimaliza kwa kuwataka Watanzania kuacha sheria ifanye kazi yake na kuwataka kuwa na imani ya Mahakama kwa kuwa ni muhimili wake unaojitegemea na hauwezi kuingiliwa.

No comments:
Post a Comment