Polisi Amuua Mkewe kwa Risasi na Kisha na Yeye Kujitandika Risasi
Askari Polisi Stephen Mungai Kinuthia wa jimbo la Nakuru nchini Kenya, amemuuwa mkewe kwa kumpiga risasi kichwani na kisha kujiua mwenyewe mbele ya mtoto wao ambaye alishuhudia tukio zima.
Kinuthia ambaye alikuwa skari polisi wa kituo cha Molo, amempiga risasi mpenzi wake huyo mara tatu kwa kutumia bunduki ya AK47 wakiwa nyumbani kwao.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mlinzi wa eneo hilo amesema walisikia kelele za watu wakilumbana, na walipokuwa wakikimbilia kujua kulikoni walisikia milio ya risasi na kisha kukawa na ukimya.
Majirani wa eneo hilo wamesema walisikia kelele za mtoto akilia kwa sauti huku akisema baba anamuuwa mama.
OCPD wa Nakuru Joshua Omukatta amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku miili ya marehemu wote ikiwa imepelekwa katika hospitali ya serikali ya Nakuru.
No comments:
Post a Comment