Mzee wa Upako: Wote Walionichafua WATAKUFA Mwakani......Wasipokufa Ntaanza Kuuza Gongo

Mzee wa Upako: Wote Walionichafua WATAKUFA Mwakani......Wasipokufa Ntaanza Kuuza Gongo

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. 

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,”alisema.

“Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi nina nguvu saaana,”alisema.

Hata hivyo baadaye mchungaji huo alishuka na kusema anamuachia Mungu wake ambaye atawahukumu kwa wakati wake.

“Lakini Mungu anasema tusihukumu, namuachia Mungu atawahukumu kwa wakati wake, haleluya, haleluya, Mungu awabariki sana."

Novemba 24, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani huyo ambaye anasikika sauti.

Taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kiroho zilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia tukio hilo, kuandika kwa urefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Novemba 26, Mzee wa Upako kwa mara ya kwanza alisita kuzungumzia sakata hilo na badala yake akasema wanaomtuhumu waendelee kusema: “Sisemi, lakini siogopi kwenda jela mimi na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”

Novemba 28, pia Mchungaji huyo akajibu akisema maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye biblia na kwamba watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.

Jana, mchungaji huyo aliwahakikishia waumini wake akisema waandishi walioandika kwa lengo la kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Katika mahubiri yake yaliyojengwa na msingi wa Biblia kutoka kitabu cha Samweli wa kwanza, sura ya 16, mstari wa saba, Mzee wa Upako aliyekaribishwa kwa nyimbo kadhaa ikiwamo ‘kusanya kusanya’ alisema yeye siyo mchungaji anayejikweza, lakini baadhi ya wachungaji wakubwa kutoka nje wamekuwa wakienda kuomba upako.

Pia, alisema hata Rais John Magufuli hakumuita yeye bali aliona kitu ndani yake na kubarikiwa kabla ya kumtembelea.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages