Picha: Mama Janeth Magufuli Alivyoshiriki ibada kwa mara ya kwanza tangu atoke hospitali

Picha: Mama Janeth Magufuli Alivyoshiriki ibada kwa mara ya kwanza tangu atoke hospitali

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli jana Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.
Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walisali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo walielezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na walimuombea afya njema.

“Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia” alisema Mama Mabula.

“Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu  Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara”alisema Thomas Simon.

Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.

Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages