Serikali kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara

Serikali kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo mbioni kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara nchini ili kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kupata leseni hizo kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati anafungua mkutano wa wadau wa kuendeleza maeneo tengefu ya viwanda vya usindikaji wa vyakula nchini.

Makamu wa Rais amesema mpango utaenda pamoja na kupunguza baadhi ya kodi na tozo ambazo ni kero kwa wananchi hasa wenye viwanda kama hatua ya kukuza biashara na uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.

Amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na wenye mabenki hususani benki ya TIB ili kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wawekezaji wenye nia ya  kuanzisha viwanda.

Kuhusu usindikaji wa bidhaa nchini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amepongeza jitihada zinazofanywa na wasindikaji wadogo nchini katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zitakidhi katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Serikali inafarijika sana kuona kuwa wasindikaji wadogo nchini wamethubutu na wana uwezo wa ushindani katika biashara ya ndani na hata nje, hivyo tunayohaki ya kujigamba kwa kuthubutu, Tumeweza na Tuendelea Kusonga mbele”

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema umefika wakati kwa Wizara na taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo kuona umuhimu wa kuhakikisha viwanda vinajengwa vijijini ili mkulima mdogo anapolima awe na uhakika wa kupata soko katika viwanda hivyo.

Amesema kuwa hali hiyo itaondoa changamoto ya kusafirisha bidhaa nyingi ambazo zinaharibika njiani au zinapofika sokoni na hivyo kukosesha jamii kipato kilichotarajiwa.

Makamu wa Rais pia amehimiza watafiti nchini wajielekeza katika kufanya tafiti ambazo zitasaidia sekta binafsi na serikali kwa ujumla kuhusu namna bora ya kukuza sekta ya viwanda nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amekiri kuwa bado kuna changamoto kubwa ya maeneo ya yatakayojengwa  viwanda na kwamba Serikali imeliona tatizo hilo na inalifanyia kazi ambapo tayari  imeshaziagiza Halmashauri zote nchini kujenga maeneo kwa ajili ya viwanda.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages