Sherehe za Maulid: Waziri Nchemba awataka Watanzania kuwafichua watu wanaotumia dini kufanya vurugu

Sherehe za Maulid: Waziri Nchemba awataka Watanzania kuwafichua watu wanaotumia dini kufanya vurugu

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania wote nchini kuungana kwa pamoja na kuwataja watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya vurugu kwa kuhusisha vitendo hivyo na dini kwani watu hao wanaweza kusababisha nchi kupoteza amani.

Waziri Nchemba ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida ambapo alisema mtu ambaye anamcha Mungu hawezi kuwa akijihusisha na vitendo hivyo na Serikali ya awamu ya tano itakuwa ikimchukulia hatua mhusika bila kuhusisha dini.

“Wizara yangu inahusika na taasisi zote zinazohusika na ibada, niwambie jambo moja tutofautishe udini na kumcha Mungu, mtu anaposhika sana dini ni mshika dini na mtu unanayemcha Mungu ni mchaMungu sio mdini, makosa yote katika nchi yanafanywa na makundi mawili ya watu wenye dini na wasio na dini,

“Kosa lolote ambalo likifanywa liwe kosa la ambae alifanya kosa, sio kosa la dini, akifanya Mkristo kosa la mtu sio la dini, akifanya Mwislamu kosa ni lake si la dini, na hata kama hana dini kosa ni lake yeye, na tusaidiane kuwa tunawafichua wanaosababisha vurugu,”amesema Nchemba.

Pia Nchemba ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa amekabidhi msaada wa mabati 1,000 kwa ajili ya kutumika kujenga misikiti na kuahidi kuwa baada ya wiki moja atawapatia gari aina ya Noah.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages