Vodacom Tanzania Na WCB (Wasafi) Waja Na ‘Nogesha Upendo’
Katika muendelezo wa kuwapatia wateja wake na watanzania wote kwa ujumla burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wasanii wa WCB imeandaa matamasha mawili ya kukata na shoka ambayo yatafanyika katika msimu huu wa sikukuu katika Mikoa ya Dar es Salaam na Iringa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyomella, alisema matamasha hayo makubwa ya muziki wa kizazi kipya yatafanyika katika mikoa ya Dar e salaam na Iringa chini ya wasanii Diamond Platinumz, Rayvanny, Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.
“Kama mnavyoelewa msimu huu huwa umeambatana na shamrashamra mbalimbali za sikukuu na mitoko ukiwa na familia yako, Desemba 24 kutashushwa shoo ya nguvu katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Hotel ambapo kutakua na tamasha la kihistoria la “Vodacom Wasafi Beach Party” na Iringa tamasha litafanyika siku ya Krismasi katika uwanja wa Samora na matamasha yote yataanza saa nane mchana”. Alisema.
Mwiyombella alisema burudani hii ya muziki inakwenda sambamba na promosheni ya “Nogesha Upendo” http://vda.cm/nogeshaupendo ya Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha haya makubwa katika msimu huu wa sikukuu.
“Ili kujishindia tiketi ya bure anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni kupiga*149*01# kisha nunua kifurushi chochote cha Vodacom na moja kwa moja atakua ameingia katika droo ya kuweza kujishindia tiketi. Zawadi nyingine kemkem kupitia promosheni ya Nogesha Upendo ni fedha taslimu, muda wa maongezi, Vifurushi vya intaneti (Mb)”.Alisema.
Naye Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika anga za kimataifa, Diamond Platinumz akiongea kwa niaba ya wasanii wa WCB alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya shoo hizo kwani zitakuwa ni shoo za kihistoria katika mikoa hii miwili kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB,Napenda kuwahakikishia mashabiki wetu kwamba tutakamua vilivyo tukiwa na wasanii wenzangu wote wa WBC kwa “Kunogesha Upendo” Alisisitiza Diamond.
No comments:
Post a Comment