Vodacom yawatengea wateja wake Bilioni 5/- kupitia promosheni ya NOGESHA UPENDO msimu huu wa Sikukuu.
Wateja wa Vodacom Tanzania wameletewa promosheni mpya inayojulikana kama “Nogesha Upendo” ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi za fedha taslimu, muda wa bure wa maongezi na vifurushi vya intaneti kila siku katika msimu huu wa sikukuu.
Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja ambapo wateja wapatao 500 wataweza kujishindia shilingi milioni 1( Tshs 1,000,000) kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema “Vodacom Tanzania tunayo furaha kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya Nogesha Upendo inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu.
Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo, tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na Data kila siku.”
Promosheni hii itawezesha wateja wetu 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1/- katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000/- katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hii”.
Aliongeza kusema “Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet,wateja wa Vodacom pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha.Kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikuu”.
Kwa ujumla, Vodacom imetenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5/- kwa ajili ya kuzawadia wateja wake kwa njia ya fedha taslimu, muda wa maongezi na bando za intaneti (MB) .Promosheni hii itakayodumu kipindi cha miezi 2 kuanzia leo ni kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom ambao laini zao ziko hewani na watakanunua vifurushi vya kupata huduma mbalimbali za kampuni.
“Promosheni ya Nogesha Upendo imebuniwa kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono muda wote,Tunawatakia heri katika msimu wa sikukuu na tunawakumbusha wakati wote kufuatilia zawadi watakazokuwa wanazishindia kutoka mtandao wa Vodacom kuanzia muda wa maongezi na fedha taslimu zitakazowawezesha kufurahia sikukuu pamoja na familia zao na marafiki. Hivi ndivyo Vodacom tumejizatiti kufanya Maisha ya wateja wetu kuwa murua na kusambaza upendo.” Alisisitiza Mworia
No comments:
Post a Comment