Chapa Kazi Kwenye Kifaa Chochote Na Mahali Popote Ukiwa Na Microsoft Office 365
Ulishawahi kukosa dili la hela kwasababu umepata dharura na ukashindwa kukamilisha kazi kwa wakati? Microsoft wanakwambia tumia kifaa chako mahali popote ulipo kupitia program ya Office365 kukamilisha mipango yako ya kibiashara au kiofisi, usikubali kupitwa na chochote.
Uwe mtandaoni au la, uwe ofisini au nje ya ofisi, ukitumia kompyuta au simu yako ya mkononi yenye program endeshi ya Android, iOS au windows unapata unachohitaji muda wowote na mahali popote.
Kupitia vifurushi vingi ya Office365, utaweza kuweka program zilizotoka hivi karibuni za Microsoft Office kwenye vifaa vyako vya kazi hivyo kukuwezesha kufanya kazi ukiwa mtandaoni au usipokuwa mtandaoni.
Programu za Office365 huboreshwa mara kwa mara na ni rahisi kuzitumia na zinakuwezesha kufikia malengo yako ya kazi.
Kuna vifurushi tofauti kulingana na mahitaji yako. Tuangalie kimoja baada ya kingine.
1. ESSENTIAL – Barua pepe, program za Office mtandaoni na usalama wa kutunza taarifa zako mtandaoni
Kifurushi hiki kinakupatia;-
- Barua pepe yenye domain yako mfano blogger@jinalakampuni.co.tz
- GB50 kwa ajili ya kuhifadhi barua pepe
- Unapata kuwekewa programu za Microsoft Office kwenye Kompyuta mpakato au simu yako
- 1TB kuhifadhi mafaili mtandaoni
2. PRODUCTIVITY – Kuwekewa full package ya programu za Office kwa ajili ya biashara yako na kuhifadhi taarifa zako mtandaoni
Kifurushi hiki kinakupatia;-
- Programu za Office 2016 kuingizwa hadi kwenye Kompyuta 5
- Kupata program za Office mtandaoni
- Kupata program za Office kwenye simu za mkononi
- 1TB kuhifadhi mafaili mtandaoni
3. PREMIUM – Unapata barua pepe, program za Office mtandaoni na usalama wa kuhifadhi mafaili
Kifurushi hiki kinakupatia vyote ambavyo unakipata katika vifurushi viwili vilivyoangalia hapo awali isipokuwa ukiwa na kifurushi kipi unapata vingine vingi vya ziada.
- Kukufanyia masuala yote ya kiufundi, vile vile wataisaidia timu yako ya kazi kuunganisha Kompyuta zao. Yote haya yanafanyika ndani ya muda mfupi sana.
- Una data nyingi kuzidi kipimo? Zungumza na Microsoft BURE na watakupatia gharama zote za kuhamisha data na kuzihifahdi kwa usalama mtandaoni – hivyo kukuwezesha kufanya kazi popote na kifaa chochote
- Msaada wa Bure: Wanapatikana kwa njia ya simu muda wa kazi ambao ni Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku kupitia mfumo maalum wa tiketi ili kukusaidia.
Kwa Maelezo na taarifa zaidi tafadhali tembeleahttp://bit.ly/barua_pepeyabiashara au piga simu namba 0784 987363 / 0715 247365 / 022-2127641 au tuma barua pepe kwendasales@extremewebtechnologies.com
No comments:
Post a Comment