China yaunda sheria mpya ya usajili, klabu kusajili wachezaji 3 tu kutoka za nje ya China
Tevez ni mmoja kati ya wachezaji waliosajiriwa kwa pesa nyingi
Timu pia zitatarajiwa kuwataja wachezaji wa China wawili wenye chini ya umri wa miaka 23 katia kikosi chao, na mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 23 katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 na shirikisho la soka la China.
Pia kuzingatia ada ya kuwasaini wachezaji kinyume cha sheria katika uhamisho wa hivi majuzi.
Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar na John Mikel Obi wameihamia China mwezi huu, huku mshambuliaji wa Manchester United na Machester City Carlos Tevez, akiripotiwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ulimwenguni alipojiunga na Shanghai Shenhua mwezi Disemba.
Shenhua ni klabu miongoni mwa klabu itakayo kabiliwa na sheria hiyo mpya, kwani klabu hiyo inawachezaji sita ambao si raia wa uchina katika kikosi chake.
Klabu hiyo inawachezaji kama vile Tevez, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba na mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Obafemi Martins
Costa amehusishwa na uhamisho wake wa kwenda Tianjin Quanjian, aliyemsahihi kiungo wa kati Axel Witsel kwa mshahara wa zaidi ya pauni milioni 15 kwa mwaka, mwezi huu wa Januari.
No comments:
Post a Comment