AFCON Yaanza kwa sare sare
Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2017) imeanza usiku wa jana kwa kushuhudia sare mbili ikiwemo ya mwenyeji Gabon ambaye amelazimishwa sare ya bao 1-1 na Guinea Bissau katika mchezo wa ufunguzi
Guinea Bissau walisawazisha bao la Aubameyang lililofungwa dakika ya 51 kunako dakika ya 89 kupitia Soares
Katika mchezo wa pili, Cameroon pia imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Burkina Faso.
Leo zinapigwa mechi mbili ya kundi B, ambapo saa 1:00 jioni Algeria inakipiga na Zimbabwe huku Tunisia ikikipiga na Senegal saa 4:00 Usiku.
No comments:
Post a Comment