Kauli ya Rais Magufuli Baada Ya CCM Kushinda Kwa Kishindo Uchaguzi Mdogo wa Marudio

Kauli ya Rais Magufuli Baada Ya CCM Kushinda Kwa Kishindo Uchaguzi Mdogo wa Marudio

Mwenyekiti  wa Taifa wa CCM, Rais John Magufuli amesema ushindi wa CCM wa ubunge na madiwani katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika juzi nchini ni ishara ya ushindi wa chama chake katika uchaguzi ujao kutokana na wananchi kuonesha imani kwake na serikali yake.

Rais Magufuli aliyasema hayo kwa waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kumpokea Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan aliyefika Ikulu, Dar es Salaam jana akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili nchini.

Rais Magufuli alisema ushindi huo ni kipimo cha utendaji wake kwa wananchi na hivyo umemuongezea ari ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wake bila ya kujali changamoto mbalimbali zilizopo.

“CCM Oyee! Mnaonaje ushindi wa CCM? Hii inadhihirisha ni namna gani wananchi walivyo na imani na mimi na serikali yangu. Tumeshinda ushindi wa kishindo katika kata na Jimbo, wenyewe mmeshuhudia namna tulivyowapiga. Au mnasemaje?” Rais Magufuli aliwaambia waandishi wa habari na kisha akawashukuru na kuelekea eneo lake maalumu akimsubiria Rais wa Uturuki kwa ajili ya kumpokea.

CCM mbali ya kushinda kiti cha ubunge cha Dimani visiwani Zanzibar, imeshinda kata 18 kati ya kata 20 zilizofanya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani juzi kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kufa kwa waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo na kufutwa kwa matokeo kwa amri ya mahakama.

Kata ambazo CCM imeshinda ni Nyarenanyuki (Arumeru, Arusha), Isegehe (Kahama, Shinyanga), Nkome (Geita), Kiwanja cha Ndege (Manispaa Morogoro), Lembeni (Mwanga, Kilimanjaro), Ihumwa (Dodoma), Matevez (Meru, Arusha), Kimwani (Muleba, Kagera), Igombavanu (Iringa), Kijichi (Mbagala, Dar es Salaam), Ng’hambi (Dodoma), Kinampundu (Singida), Kasansa (Katavi), Malya na Kahumulo (Mwanza), Mkoma (Mara), Misugusugu (Kibaha, Pwani).

Aidha, CCM imeshindwa katika Kata ya Duru mkoani Manyara, ambako mgombea wa Chadema, Ali Shaaban ameibuka mshindi.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages