Sakata la Baa la Njaa: Zitto Kabwe Atishia Kujiuzulu Ubunge Serikali Ikiwa na Tani Milioni 1.5 za Mahindi

Sakata la Baa la Njaa: Zitto Kabwe Atishia Kujiuzulu Ubunge Serikali Ikiwa na Tani Milioni 1.5 za Mahindi

Baada ya kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupaza sauti kuhusu hali ya chakula nchini huku akisema kuwa serikali haina chakula cha kutosha, viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wameibuka na kusema kuwa si kweli kwamba nchi imekumbwa na njaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba ni kuwa serikali ina akiba ya chakula cha kutosheleza. Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza juzi  mjini Dodoma aligiza Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula kusambaza chakula nchini ili kudhibiti kupanda kwa bei ya vyakula maeneo mbalimbali.

Jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mbunge Zitto Kabwe aliandika maneno haya;

"Serikali ya CCM ikinionyesha tani 1.5m za chakula kutoka Hifadhi ya Taifa ya Chakula ambazo inataka kusambaza najiuzulu Ubunge mara moja.
 
Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu Hivi kwenye maghala yote ya NFRA.

Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu.

Nimesikia Mwenezi wa CCM ameongea na waandishi Leo. Natarajia ndugu Ado Shaibu atamkaribisha mwenzake ulingoni"- Zitto Kabwe
 

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages