UVCCM yawataka wananchi kuwapuuza Lowassa na Sumaye........Yadai Si Waadilifu, Wanasaka Madaraka
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umewataka watanzania kuwapuuza Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward lowassa kuwa wanaota ndoto za mchana .
Umoja huo umesema kuwa kuiombea CCM kushindwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni sawa na kujivisha akili za Abunuasi,ambaye mipango haitimii, aidha umoja huo umesema upinzani wa Tanzania haukubaliki mbele ya wananchi wazalendo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni katika kata ya kiwanja cha ndege mkoani Morogoro.
Alisema kuwa wananchi hawana budi kuwapuuza Lowassa, Sumaye na chama chao kwa sababu sio viongozi waadilifu bali ni wasaka madaraka.
“Watanzania wapuuzeni watu hawa kwa sababu Sumaye ni Pwagu na mwenzake Lowassa ni pwaguzi, wanahaha usiku na mchana kusaka madaraka wakati wananchi wanawajua sio waadilifu na hawaaminiki katika jamii,”alisema Shaka.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini,Fikiri Juma na Kaimu Katibu Mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge.
No comments:
Post a Comment