Zitto Kabwe: Watanzania wakifa njaa Tutaiwajibisha Serikali kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A

Zitto Kabwe: Watanzania wakifa njaa Tutaiwajibisha Serikali kwa mujibu wa Katiba ibara ya 46A

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema endapo Mtanzania yeyote atakufa kwa njaa watachukua jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake.

Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kijichi jana,  kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto alisema, “Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshtaki kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais. "

Kauli hiyo ya Zitto ilitokana na msimamo wa Rais Magufuli kuwa hakuna njaa nchini na kwamba Serikali haitatoa chakula cha msaada, huku makundi mengine ya wananchi, wakiwamo  wanasiasa na viongozi wa dini wakisema kuna upungufu wa chakula uliotokana na ukame. 

Zitto ambaye kabla ya kuhutubia alipita nyumba za jirani na uwanja akisalimia, alisema, “Tumesema hili la njaa katika kutekeleza wajibu wetu, Rais na Serikali wamejibu na kufunga mjadala. Wakati utaamua na kuonyesha mkweli nani na mpiga propaganda nani.” 

“Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake, Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani. 

“Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao,” aliongeza. 

Alisema Rais yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi kulinda Katiba, anaweza kuwa wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. 

“Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni,” alisema. 

Mbunge huyo alitoa wito kwa Watanzania bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. 

Alimtaka Rais atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana. 

Kiongozi huyo alisema ameamua kusema hayo kwa sababu baada ya siku saba hawatakuwa na nafasi ya kuzungumza majukwaani kama viongozi wa vyama vya siasa kwa sababu ya zuio lisilo la kikatiba la kuzuia mikutano ya hadhara. 

Hata hivyo, sheria inasema janga la njaa linaweza kutangazwa na Rais tu na si mtu mwingine.
 

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages