Makamu wa Rais Samia Suluhu kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu

Makamu wa Rais Samia Suluhu kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu lililopo Iringa kutokana uharibifu mkubwa unaendelea, huku akiambatana na Mawaziri watano ambao watasaidia kuokoa uharibifu wa Mazingira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.

Alisema kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za kiuchumi.

Aidha, Makamba aliwataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.

Vile vile, aliongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.

“Hali hii inasababisha kupungua kwa watalii, shughuli za kiuchumi na uzalishaji wa umeme ambao unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema nafuu, pia uhalibifu huu wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,”alisema Makamba.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages