Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Kwa Mwezi Machi 2017 Umeongezeka Hadi Kufikia Asilimia 6.4

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Kwa Mwezi Machi 2017 Umeongezeka Hadi Kufikia Asilimia 6.4

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2017 umeongeza hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.5 mwezi Februari 2017.

Hayo yalibainishwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam naja.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi wa Februari 2017.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.44 mwezi Machi 2017 kutoka 101.93 mwezi Machi 2016.Mfumuko wa Bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi 2017 umeongezeka hadi asilimia 11.0 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Februari 2017.

Taarifa hiyo imeonesha kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Machi 2017 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2016.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages