Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Alivyosherehekea Siku yake ya Kuzaliwa Ambayo Ilikuwa ni Jana April 9

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Alivyosherehekea Siku yake ya Kuzaliwa Ambayo Ilikuwa ni Jana April 9

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli jana  aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa Watanzania kusaidia watu wenye mahitaji.

Akiwa hospitalini hapo, Mama Magufuli, alisema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa huu ambapo pia alipata fursa ya kuwaombea afya njema wagonjwa wote na kuwatia moyo ndugu wanaouguza kuendelea na jukumu hilo zito.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage alimshukuru  Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia wagonjwa hospitalini hapo kwa kuwa kitendo hicho kinawatia moyo wao kama wauguzi lakini pia kinarudisha imani kwa wagonjwa na kujiona kuwa hawapo peke yao.

Mama Janeth Magufuli kwa kushirikiana na wanawake wa Wilaya ya Ilala na Temeke wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema walitoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mchele, maharage, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea, maziwa ya unga,juisi, taulo za kike, vitenge, kanga, misuli,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages