Mchungaji Amfananisha Rais Magufuli na Nabii Mussa
RAIS Dk. Jonh Magufuli amefananishwa na Nabii Mussa wa kwenye Biblia, aliyekuja kuwaokomboa wana wa Israel kutoka Misri.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mchungaji wa Kanisa la IEACT la mjiniShinyanga, David Mabushi, alipokuwa akizungumza na mwandishi, baada ya Misa ya Pasaka, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu mustakabali wa taifa.

"Mimi na kanisa langu tunamuunga mkono kwa kazi zote anazofanya kwa kusaidia rasilimali zote za nchi hii ill ziwanufaishe Watanzania. Huyu ni kama Mussa aliyekuja kuwakomboa wana wa Waisraeli,"alisema Mabushi.
Alisema miongoni mwa mambo, ambayo Watanzania walikuwa wanalalamikia ni mikataba ya migodi na mchanga unaosombwa kupelekwa nje ya nchi, ambayo kwa sasa yameanza kushughulikiwa.
"Hivi sasa kazuia na kuunda tume mbili. Moja ya wataalamu wa kujua kilichomo ndani ya mchanga na nyingine ina wachumi na wanasheria watakaoangalia mikataba inasema nini," alisema.
Pia, aliwakumbusha Watanzania kauli ya Baba wa Taifa, aliyoitoa siku za nyuma kuwa, mali ya nchi hii haiozi, ataiweka mpaka wasomi waje.
Hata hivyo, mchungaji huyo alielezea kusikitishwa kwake na kushuka kwa maadili ya watoto wanaotumia mitandao kuangalia mambo machafu, badala ya kuitumia kujifunza.
Kuhusu mauaji ya askari, alisema anaungana na serikali kulaani mauaji hayo.
Kuhusu mauaji ya askari, alisema anaungana na serikali kulaani mauaji hayo.
"Naiomba serikali itunishe misuli na kuhakikisha wale wote waliohusika na mauaji hayo, wanapatikana na kufikishwa mahali panapohusika," alisema.
No comments:
Post a Comment