Kikosi cha Simba wako vizuri kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, keshokutwa.
Simba wako tayari kwa mechi hiyo na kesho watafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini humo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mechi.
“Mechi ni ngumu tena sana na Kagera ni timu nzuri, tunalitambua hilo. Lakini tumejiandaa na tupo tayari. Sasa ni maandalizi ya mwisho na wachezaji, makocha na wengine tunataka kushinda,” alisema.
No comments:
Post a Comment