Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Atiwa Mbaroni

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Atiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali mwilini.
 
Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, alikamatwa  jana mchana
 
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi, alisema kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita.
 
Akifafanua, Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta.
 
"Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu, tumemkamata leo(jana)  saa nane mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake,"alisema Mjengi na kuongeza:
 
"Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa, walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwanamke huyo hajui ni ya kitu gani," alisema Mjengi.
 
Alipohojiwa zaidi, Mjengi alikataa kuweka wazi jina la mwanamke na idadi ya watuhumiwa wengine kwa maelezo kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu upelelezi unaoendelea.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages