Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime
MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia.
Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katikamiradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato.
Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake kijiji cha Itiryo kusherekea sikukuu ya Pasaka.
Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ujumla.
Alisema awali, wilaya hiyo ilikuwa na sifa mbaya nchini na kimataifa, kutokana na kuzuka kwa mapigano ya koo za makabila ya Wakurya na Waluo, yaliyochochewa na wizi wa mifugo.
Waitara alisema ipo haja kwa jamii inayoishi kando ya Hifadhi ya Serengeti, kuthamini rasilimali za wanyamapori kuwa ni miongoni mwa tunu za taifa na hakuna budi kuzitunza na kuzilinda kwa ajili vizazi vya sasa na vijavyo.
"Ni muhimu jamii yetu itambue kuwa, wanyama waliopo ni wetu kwa faida yetu na taifa la leo na vizaz vijavyo. Kuendekeza uwindaji haramu kunasababisha hasara kubwa dhidi ya rasilimali hiyo, hivyo ni muhimu jamii yetu ikatumia fursa zilizopo katika utalii ili kunufaika nazo,"alisema.
"Ni muhimu jamii yetu itambue kuwa, wanyama waliopo ni wetu kwa faida yetu na taifa la leo na vizaz vijavyo. Kuendekeza uwindaji haramu kunasababisha hasara kubwa dhidi ya rasilimali hiyo, hivyo ni muhimu jamii yetu ikatumia fursa zilizopo katika utalii ili kunufaika nazo,"alisema.
Kuhusu miradi ya kijamii inayoibuliwa na vijiji na kisha kupitishwa na kamati za maendeleo za kata, kama vipaumbele vyao vya kutekelezwa na Hifadhi ya Mbuga ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), alisema utekelezaji wake utasubiri kutokana na bajeti ya hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment