CHADEMA wataka Rais Mkapa anyang’anywe shamba kama Sumaye
Meya wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa shamba linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama alivyofanya kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Meya huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake wanamiliki shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu sasa.
Meya huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba hilo lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili liweze kufanyiwa shughuli nyingine.
Hoja hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.
Meya alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la mwananchi ambapo alisema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba abatilishe umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo kwanza imeanzishwa.
No comments:
Post a Comment