Simba vs Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017, bye bye Yanga
Usiku wa January 10 2017 visiwani Zanzibar mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Mapinduzi Cup 2017 kati ya Simba dhidi ya Yanga ulichezwa visiwani Zanzibar katika uwanja wa Amaan, baada ya Azam FC kutinga hatua ya fainali kwa kumfunga Taifa Jang’ombe goli 1-0.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Simba kukutana na Yanga wakiwa na kocha wao mpya mzambia George Lwandamina ambaye aliiwezesha Zesco United ya Zambia kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Yanga na Simba kwa dakika 90 zilimalizika pasipo kufungana, hivyo ililazimika kupigwa mikwaju ya penati ili kupata mshindi atakayecheza fainali na Azam FC Ijumaa ya January 13 2017, Simba wamekuwa vinara kwa Yanga kwa kuifunga kwa penati 4-2.
Deogratus Munish na Haji Mwinyi ndio waliyokosa penati kwa upande wa Yanga wakati Simba akikosa penati mchezaji wao bora wa mechi mara mbili mfululizo Method Mwanjale, kiungo mghana James Kotei ndio ameibuka mchezaji bora wa mechi kwa leo.
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4
No comments:
Post a Comment