Waziri Simbachawene 'ANYWEA' kuhusu Zoezi la Kuwaondoa Machinga
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mhe. George Simbachawene ameitikia mara moja agizo lililotolewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli la kusitisha zoezi la kuwaondoa machinga maeneo yasiyo rasmi
Mhe. Simbachawene, ameitikia agizo hilo kwa kuwataka wakuu wa wilaya pamoja na halmashauri zote nchini kuangalia ufumbuzi na utaratibu mzuri wa kuwashirikisha wajasiriamali hao ili kupata ufumbuzi ulioshirikisha kuliko utaratibu wa sasa wakuwafukuza bila kusikiliza madai yao.
Mhe. Simbachawene amesema, Rais Magufuli anatambua mchango mkubwa na kazi nzuri inayofanywa na wakuu wa wilaya katika kuleta maendeleo hivyo kuweka maeneo sahihi kwaajili ya wafanyabiashara wadogo kutaleta maana kubwa ya uwajibikaji.
“Kwa kuanzia ni vema yakatengwa maeneo ya katikati ya mji yenye wateja wa bidhaa zinazouzwa, kwa kuangalia uwezekano wa kufunga mtaa japo mmoja ili utumike kwa kazi za kimachinga,” alisema jana Simbachawene wakati akiongea na waandishi wa habari.
Alisema usumbufu unaojitokeza maeneo mbalimbali unasababisha wananchi kupoteza mitaji yao ambayo wengine wamekopa kwenye vikundi vya vicoba na hivyo kuhatarisha mustakabali wa maisha yao na familia zao.
Alisema usumbufu unaojitokeza maeneo mbalimbali unasababisha wananchi kupoteza mitaji yao ambayo wengine wamekopa kwenye vikundi vya vicoba na hivyo kuhatarisha mustakabali wa maisha yao na familia zao.
Hivi karibuni waziri huyu alitoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchi nzima kuhakikisha wanawaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi kwa sababu wanaleta usumbufu na uchafu,agizo ambalo lilianza kutekelezwa mara moja katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mwanza na Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment