Isikilize Video ya Rais Magufuli Akiwapiga Marufuku Wakuu wa Mikoa Kuwasumbua Machinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.
Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.
No comments:
Post a Comment