Goal inakuletea mambo manne tuliyojifunza Tanzania na Botswana

Tanzania 2-0 Botswana : Mambo manne tuliyojifunza
Timu ya Tanzania, Taifa Stars chini ya mwalimu mpya Salumu Mayanga wamefanimiwa kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila dhidi ya Botswana kwenye mechi ya kirafiki.
Tanzania ambao ndiyo walikuwa wenyeji kwenye mchezo huo, ili wachukua dakika mbili tu za kipindi cha kwanza kupata goli lililofungwa na nyota wa Genk Mbwana Samatta.
Kwa muda mwingi wa mchezo, stars walionekana kuwazidi Botswana karibu kila idara uwanjani na walifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo hawa kuzitumia vizuri huku Samatta na Msuva wakikosa nafasi mbili za wazi.
Wakati mpira ukielekea kumalizika, Samatta aliwatungua tena Wabotswana hao kwa mpira wa adhabu ndogo ambao ulizama moja kwa moja.
Goal inakuletea mambo manne tuliyojifunza Tanzania na Botswana.
1. Kuna kazi kubwa ya stars kufuzu CHAN mwakani Kenya
Kikosi cha taifa stars chini ya Mayanga, kwa asilimia kubwa bado kina tegemea nguvu ya Mbwana Samatta kwenye eneo la ushambuliaji hivyo kukosekana kwake Samatta kwenye CHAN kuna uwezekano wakukipa wakati mgumu kikosi cha stars kufuzu mbele ya timu ngumu kama Rwanda na Uganda.
2.Kombinesheni ya Banda na Nyoni itatugharimu  kwenye mechi za mashindano
Nyota hao wameonekana kutokuelewana kwa muda mwingi wa mchezo kwa kuingiliana majukumu uwanjani, licha ya Botswana kufanya mashambulizi machache lakini walifanikiwa kupenya ngome kirahisi kilicho waangusha ni umaliziaji mbovu, nafasi ya beki wa Mtibwa Salim Mbonde ni kubwa ndani ya kikosi cha Mayanga, anastahili kuanza badala ya Nyoni.
3.Mbwana Samatta ameonesha utofauti wake na wengine kikosini
Ili kupiga hatua kisoka nchini inabidi idadi ya wachezaji wanao sakata kabumbu nje ya nchini iongezeke, katika mchezo dhidi ya Botswana tumeona utofauti wa Samatta na wengine kuanzia kwenye kupokea mipira, kutengeneza nafasi na kutumia nafasi vizuri.
4.Botswana haikuwa timu ya kuipa upinzani mkubwa taifa stars
Kama baadhi ya wachezaji wa Tanzania wangetumia vizuri nafasi zao, kulikuwa na uwezekano wa kuibuka na ushindi wa zaidi ya goli 5 Wabotswana wali zidiwa na kuaonekana ni timu ya kawaida ambayo ilishindwa kuleta upinzani mkubwa kwa stars.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages