Mbunge wa Nzega Hussein Bashe Afunguka Maneno Mazito Kuhusu Hali ya Kisiasa Ilivyo Hivi sasa Nchini
Mbunge wa Nzega mjini kupitia CCM Hussein Bashe amepost ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno yaliyosomeka…"Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo
"Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu.
"Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru.
"Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu.
"Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu.
"Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania UHURU wa taifa letu. TUJISAHIHISHE."
No comments:
Post a Comment