Gwajima: Mimi ndo chanzo cha Nape Nnauye Kutumbuliwa na Rais
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.
Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha Efm,Gwajima amesema Mkuu wa Mkoa alivamia ofisi za Clouds kwa lengo la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.
"Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.
Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.
No comments:
Post a Comment