Mchungaji Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumbaka na Kumlawiti Mtoto
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Ipagala Manispaa ya Dodoma, Joshua Warioba, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea Machi 2, mwaka huu, majira ya jioni katika kituo cha chekechea cha Efretha English Medium Pre & Primary School, kinachomilikiwa na mchungaji huyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa Mchungaji huyo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuingilia mtoto huyo kila siku alipokuwa akienda masomo ya ziada (tuition) na jalada la kesi hiyo lipo kwa mwanasheria wa serikali ambae muda wowote atapeleka hati ya mashtaka polisi ili afikishwe mahakamani.
Mama wa mtoto huyo anasema kuwa alimwandikisha mwanae kusoma chekechea katika shule ya kanisa hilo Februari 2. Baada ya mdogo wake kuja nyumbani kwake na kuuliza kama mwanae nae huwa anahudhuria masomo ya ziada na kujibiwa kuwa hajui kama kuna masomo hayo. Ndipo alipoamua kufuatilia kwa majirani wengine pia kuubaini ukweli.
Walipomuuliza mtoto huyo alisema japo kwa woga vitendo alivyokuwa akifanyiwa na mchungaji huyo. Ndipo walipoweka mtego na kumfuma mchungaji huyo akiwa na mtoto huyo kwenye chumba huku nguo zake za ndani zikiwa zimeshushwa.
Wananchi walikusanyika wakitaka kumpiga mchungaji huyo lakini aliokolewa na mwanajeshi mmoja na kukimbizwa polisi.
Baada ya mzazi huyo kufika polisi aliandikiwa mtoto aende kupimwa hospitali na majibu ya daktari yalionyesha kuwa mtoto ana michubuko. Alipoulizwa mtoto huyo alisema kuwa mchungaji alikuwa akimbaka kila alipoenda kusoma.
Kamanda Mambosasa aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto kwenda kusoma masomo ya ziada (Tuition) pasipo kuwa na uangalizi wa karibu na pia aliitaka jamii kuendelea kupiga vita dhidhi ya matendo ya udhalilishaji kwa kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe.
No comments:
Post a Comment