Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye ambaye leo ametenguliwa na Rais Magufuli amefunguka na kusema leo mchana atakutana na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Nape Nnauye ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mchinga amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter
"Ndugu zangu naomba tutulie! leo mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba tutulie" Nape Nnauye
Rais Magufuli leo asubuhi amefanya mabadiliko madogo ya baraza lake la Mawaziri kwa kumteua Dr. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo. ambayo ilikuwa chini ya Nape Nnauye pia amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
No comments:
Post a Comment