Wajumbe wa CCM wapitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM
Wajumbe 2,356 wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM leo wamepitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM kwa kauli moja chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli
Mabadiliko hayo ya CCM yamelenga katika maeneo matatu makuu ikiwa ni pamoja na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Kanuni za Uchaguzi za CCM pamoja na Kanuni za Jumuiya (UWT, UVCCM na Wazazi)
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi amedai kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa ukiendelea kuwa mabadiliko hayo yanafanywa kwa kumlenga mtu au kundi fulani la watu na kusema huo si kweli bali wanafanya mabadiliko hayo kwa lengo la kukijenga chama.
Mbali na hilo Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli aliweka wazi lengo kuu la mabadiliko hayo ni pamoja na kuimarisha chama chao na kukufanya kiendelee kutawala na kufanya vyema siku hadi siku.
“Mabadiliko yanalenga kuboresha mfumo na muunda wa chama chetu, wa sasa una mapungufu mengi utakuta watendaji wanafanya majukumu yanayofanana na kugongana kimaamuzi, pia kuliibuka vyeo vilivyo na nguvu, watu walivitumia kwa maslahi yao binafsi japokuwa kikatiba havipo”. Alisema Magufuli
Aidha Mwenyekiti huyo alitoa onyo kali kwa mamluki yeyote atakajitokeza kuharibu mchakato huo kwa namna moja ama nyingine na kusema adhabu kali dhidi yake itachukuliwa.
No comments:
Post a Comment