Waziri Nape asema Kitendo Kilichofanywa na Makonda kimenajisi Tasnia ya Habari....... Aunda tume kuchunguza uvamizi Huo

Waziri Nape asema Kitendo Kilichofanywa na Makonda kimenajisi Tasnia ya Habari....... Aunda tume kuchunguza uvamizi Huo

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutaka apewe matokeo ndani ya saa 24.

Nape ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari  mara baada ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ujumaa usiku akiwa na polisi wenye silaha.

“Matukio kama haya hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa  basi kuingia ndani ya chombo cha habari na silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari.

"Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

"Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi

"Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya

"Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi

"Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia

"Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24." Amesema Waziri Nape

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages