Kocha Salum Mayanga, amesema anaamini Taifa Stars watajituma ili kushinda mechi dhidi ya Burundi.
Stars inaivaa Burundi katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
"Burundi ni timu ngumu, mara nyingi wana wachezaji wenye maumbo madogo lakini wenye vipaji.
"Lengo letu ni kufanya vizuri na wachezaji wanalijua hili. Kilichobaki ni kukumbushana na kuhimizana lakini tunachotaka ni kufanya vizuri," alisema.
Tayari Stars imeshinda mechi yake ya kwanza ya kirafiki chini ya Mayanga kwa kuichapa Botswana, Jumamosi iliyopita.
No comments:
Post a Comment