Pluijm ametamba kuibomoa Yanga kwa kuwasajili nyota watatu wanaofanya vizuri kwenye kikosi hicho

Ngoma na Msuva kumfuata Pluijm?
Baada ya kutua Singida United kama kocha mkuu Hans van der Pluijm, ametamba kuibomoaYanga kwa kuwasajili nyota watatu wanaofanya vizuri kwenye kikosi hicho.

Pluijm ameiambia Goal, anawataka wachezaji Donald Ngoma, Thabani Kamusoko wote raia wa Zimbabwe na Simon Msuva kwasababu anawakubali kwa kiwango walichokuwa nacho na anaamini watakuwa na msaada mkubwa kwenye kibarua chake.
Pluijm anaweza twaa ubingwa na Singida United?

“Ngoma, Msuva na Kamusoko, n ivijana wangu nimefanya nao kazi vizuri na wanaelekea kumaliza mikataba yao na Yanga na hivyo haitakuwa kazi kuwapata nyota hao,” amesema Pluijm.

Mdachi huyo amesema anajua hakuna kinachoshindikana kwa sababu Singida United ni timu kubwa na inauwezo kifedha wa kuwanasa wachezaji hao ambao wanaubora wa hali ya juu.

Amesema kama kocha amepania kuona Singida inakuwa timu ya kuogopewa msimu ujao na ikiwezekana wanatwaa ubingwa wa ligi ya Vodacom msimu ujao.

Pluijm aliyesitishiwa mkataba na Yanga siku za karibuni amewataka mashabiki wa soka Tanzania kuisubiri kwa hamu timu hiyo ili kuona namna watakavyo leta mapinduzi.

Amesema anajua watu wengi hawaipi nafasi timu yake lakini kwa kupitia uwezo wake aliokuwa nao atawashangaza watu wengi kwani wanataka ubingwa wa Tanzania Bara.

Kocha huyo tayari  amefanikisha usajili wa kiungo mchezeshaji, raia wa Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu kutoka Klabu ya Chicken Inn ya nchini Zimbabwe.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages