Gwajima Ajitosa Sakata La Vanessa Mdee...
"Sasa hapo ndio najiuliza, polisi na uhamiaji waseme kwanini wanasuasua na kuna makosa niliyoyataja angalau saba ya jinai wakati wengine wamelala ndani kwa kuhisiwa tu wakiwemo wanamuziki kwa mfano Vanessa Mdee.
"Amelala ndani tu alikuwa nje wakati sisi ametajwa naye ametajwa amerudi ndani leo siku ya tatu Vanessa Mdee leo yuko ndani kwa kuhisiwa tu.
"Lakini huyu mpaka tumetaja Daudi Bashite yupo katorokaje? Huyu kakimbiaje? Vanessa Mdee simfahamu wala simjui lakini alikuwa ana performing zake nje ya nchi kashikwa pale yuko ndani leo, huyu katorokaje? Kwanini wengine wako ndani na wengine wanazunguka mitaa ya South Africa wakati walitakiwa wawe hapa na wao, mbona mimi nilienda kulala tu?"
==>Msikilize Hapo Chini
No comments:
Post a Comment