Producer Majani amtabiria 'ufalme' Harmorapa

Producer Majani amtabiria 'ufalme' Harmorapa
Producer mkongwe nchini P Funk Majani amemtabiria msanii Harmorappa kuja kuwa msanii mkubwa nchini tofauti na watu ambavyo wanamchukulia kama kijana asiyejua chochote kwenye muziki na anayetafuta kiki huku wakimbeza kwamba hajui kuimba.

Jana wakati akiwa amemsindikiza msanii huyo kwenye kipindi cha FNL cha EATV kuzindua video yake mpya 'Kiboko ya Mabishoo', Majani amesema Harmorapa ni mtoto wa kipekee sana ambaye huonesha adabu ya hali ya juu wakati akizungumza na hata akiwa anamsikiliza mtu yeyote.

"This kid is very special', 'the way he seats and listen, the way he speaks to people', ana heshima kubwa mno ambayo mimi sijawaji kupata, anapenda kujifunza zaidi, habahatishi kama watu wanavyosema anatafuta umaarufu, he is gonna be big trust me Sam" Majani alifafanua.

Majani amesema hakuna msanii aliyeanza akiwa anajua kwa sababu wengi wamepita kwenye mikono yake na walianza kwa kutambaa mpaka leo walipofikia hivyo na kwamba hata Harmorapa naye ana uwezo wa kujifunza na kufikia sehemu kubwa zaidi.

Kuhusu suala la Harmorapa kutumia jina linalofanana na msanii ambaye wanafananishwa kimuonekano Majani amesema alikwisha mshauri abadilishe jina hilo lakini msanii huyo ameamua kukaa nalo kwa kuwa katika majina ambayo alikuwa anatumia zamani hilo la Harmorapa ndilo limeonekana kung’ara zaidi.

Kwa upande wake Harmorapa amesema ana mambo mazuri ambayo mashabiki wake wanapaswa kusubiri na siyo kiki tena kama ambavyo watu wanadhani kwani yeye amejipanga kufanya muziki mzuri.

“Siku zote ‘focus’ yangu ipo kwenye muziki wangu , watu ndio wanaopaisha hizo kiki, kuhusu kolabo na Ali Kiba siwezi kuiongelea kwa sasa lakini mapungufu yangu ya kithethe hayana matatizo kwani kila binadamu ana mapungufu yake” Aliongezea Harmorappa.



VIDEO: KUHUSU NDOA YA WEMA SEPETU
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages