Breaking News:Mbunge wa Kilombero Morogoro (CHADEMA ) ahukumiwa miezi 6 jela Bila Faini

Breaking News:Mbunge wa Kilombero Morogoro (CHADEMA ) ahukumiwa miezi 6 jela Bila Faini

Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemuhukumu kifungo cha miezi sita jela Mbunge Wa jimbo la Kilombero Peter Lijualikali (30)   kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero

Mwendesha mashtaka inspekta Wa Polisi Dotto Ngimbwa aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi mosi mwaka 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

Ngimbwa alisema washtakiwa hao kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha shtaka bila kuacha shaka.

Hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya ya Kilombero Timothy Lyon alisema mahakama imewatia hatiani kwa kosa hilo na kwa kuwa mshtakiwa Wa kwanza ni Mbunge ambaye alikuwa na kesi tatu huko nyuma na kutiwa hatiani amehukumuwa jela miezi sita.

Lyon alizitaja kesi za nyuma ambazo mbunge huyo alitiwa hatiani nakuhukumiwa ni kesi namba 338 ya mwaka 2014, kesi namba 220 ya mwaka 2014 na kesi namba 340 ya mwaka 2014, hivyo kutokana na mshtakiwa ni mzoefu katika kesi zote, mahakama imemkuta na hatia ya kwenda jela miezi sita.

Hata hivyo mahakama hiyo imeona kwa kuwa mshtakiwa wa pili Stephano Mgata (35), hii ni Mara yake ya kwanza amehukumiwa kifungo cha miezi sita nje ambapo ndani ya kipindi hicho cha miezi sita hatotakiwa kutenda kosa lolote la jinai.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida hali katika mahakama hiyo ilikuwa tulivu tofauti na kesi nyingine dhidi ya Mbunge Lijualikali, ambapo wafuasi wachache wanaodhaniwa kuwa ni wa Chadema ndiyo walijitokeza na baada ya hukumu kutolewa Mbunge huyo alipelekwa haraka gerezani kwenda kuanza kutumikia kifungo chake

Kutokana na jambo hili mwanasiasa Julius Mtatiro anasema kuwa licha ya Lijualikali kufungwa jela lakini hali hiyo haiwezi kupoteza ubunge wake na kusema kama akikata rufaa huenda akapata haki.

"Hawezi kupoteza ubunge kwa kifungo hicho na kama akikata rufaa anaweza kupata haki, Kumfunga Lijuakali kwa sababu alihoji na kupinga kunyimwa haki yake ni kuzalisha Lijualikali wengi zaidi"alisema Julius Mtatiro
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages