Aika (Navy Kenzo) afunguka haya kuhusu Vanessa Mdee
Muimbaji wa kundi la Navy Kenzo, Aika, amedai kuwa Vanessa Mdee ndiye aliyewahamasisha kurudi kwenye muziki baada ya kuwa wamekata tamaa.
“Ni msichana ambaye ana bidii, ametumotivate vitu vingi sana hata sisi kwenye maisha yetu,” amesema Aika. “Tuseme, yeye ndiye alitufanya sisi turudi kwenye muziki baada ya kuja studio na kusikiliza nyimbo zetu na kusema ‘jamani toeni hii nyimbo ya Bokodo’ by then. Alitupa nguvu sana na ni mtu ambaye amekuwa akituencourage tukisaidiana,” ameongeza.
Vee Money pia aliwahi kuzungumzia story hii.
Akizungumza kwenye kipindi cha Up Close & Personal cha K24 ya Kenya, Vee alisema alikutana na Nahree na Aika baada ya kupigwa chini na label ya B’Hits.
“Kwahiyo nikasema nahitaji kumpata mtu ambaye anaweza kupatia sauti yangu. Shout out kwa Hermy kwasababu sasa sisi ni familia, ni kaka yangu daima. Kwahiyo nilikuwa naijua hii bendi ya Navy Kenzo toka Arusha na wakati huo walikuwa wakijulikana kama Pah One. Pah One ikaja kuvunjika na wawili kati yao walikuwa wanataka kwenda nje kusoma masters, nilienda kwenye studio yao ambayo wakati huo ilikuwa nyumba yao na nikamuambia Nahreel ‘nakuaminia, nadhani mimi na wewe tunaweza kufanya mambo makubwa pamoja,’” alisema Vanesa.
No comments:
Post a Comment