Ujumbe kutoka kwa RC Makonda leo March 5
Jina la Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda sasa hivi linatajwa sana kwenye headlines za sakata la dawa za kulevya, hii inatokana na kuamua kama kiongozi kuongoza vita dhidi ya dawa ya kulevya kiasi cha kufikia hatua ya kutaja majina kadhaa ya wanaotuhumiwa.
Licha ya kuwa Paul Makonda ni kiongozi anayependa kunukuu maneno kutoka katika kitabu takatifu cha dini yake ya kikristo Biblia, anapenda pia kutumia nukuu za misemo ya wahenga ambayo inatumiwa na watu mbalimbali katika harakati za kumtia moyo mtu ili kutokata tamaa katika jambo lolote.
Asubuhi ya March 6 RC Makonda ametumia account yake ya instagram kuandika moja kati ya nukuu zinazotumiwa na watu wengi kuhamasisha kutokata tamaa ya jambo fulani.“Usiku hata uwe mrefu kiasi gani lazima asubuhi itafika…Asubuhi yako iii karibu Kaza butii..you are almost there”
No comments:
Post a Comment