CUF Wakataa Suluhu na Profesa Lipumba

CUF Wakataa Suluhu na Profesa Lipumba

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitafanya mazungumzo kusaka suluhu na mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kwamba, kipo tayari kwa lolote hata kama kitafutiwa usajili.
 
Aidha, chama hicho kimesema hakijutii kumkaribisha na kumuunga mkono Edward Lowassa, ambaye aliteuliwa kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema na kuwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
 
Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF,  Mbarala Maharagande kujibu madai yaliyotolewa na Profesa Lipumba alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha televisheni hapa nchini.
 
Katika mahojiano hayo, Profesa Lipumba alidai kuwa mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sasa hautamalizwa na mahakama pekee bali viongozi wa pande zote mbili wanatakiwa kuzungumza, lakini Maharagande amesema haiwezekani kwa vile Lipumba alishakwisha kukivuruga chama na hafai tena kuendelea kuwa kiongozi.
 
“Lipumba anasema tukae tulimalize suala hili kwa kuongea sisi wenyewe. Jambo hilo haliwezekani kwa kuwa kama kupandikiza chuki, uhasama, uharibifu wa chama miongoni mwa wanachama na viongozi ameshafanya na kufanikiwa hilo kwa baadhi ya wanachama na viongozi wake na kuharibu taswira ya chama kwa jamii,” amesema Maharagande.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages