Pwani: Bunduki Ya Kivita SMG Iliyokuwa Imeibiwa na Mfanyakazi wa Hifadhi ya Saadani Yakutwa Kichakani

Pwani: Bunduki Ya Kivita SMG Iliyokuwa Imeibiwa na Mfanyakazi wa Hifadhi ya Saadani Yakutwa Kichakani

Silaha ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 

Silaha hiyo inadaiwa iliibiwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini. 

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bonaventura Mushongi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka zamu ya lindo la geti hilo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo. 

“Huyu askari alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana zamu ya ulinzi hivyo alitoka na silaha yake akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi na ndipo ilipoibiwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi hiyo,” alisema. 

Mushongi alibainisha kuwa baada ya wizi huo, askari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) walianza msako na kupitia taarifa ya msamaria mwema walimkamata mtuhumiwa huyo, mkazi wa Tegeta Kibaoni ambaye alikwenda kuonyesha alipokuwa ameificha kichakani ikiwa na risasi 30. 

Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk James Wakibara alisema wameshtushwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea na kwamba, zaidi ni baada ya kukuta mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa mtumishi wao na aliacha kazi miezi kadhaa iliyopita yeye mwenyewe. 

Dk Wakibara alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano lilioutoa toka siku ilipoibiwa silaha hiyo hadi ilipopatikana.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages