Wizara 7 Vitani Sakata la Uvuvi Haramu

Wizara 7 Vitani Sakata la Uvuvi Haramu

Kukithiri kwa uvuvi haramu hasa wa kutumia mabomu kumesababisha mawaziri wa wizara saba kukutana ghafla ili kujadiliana namna ya kukabiliana na tatizo hilo. 

 Mawaziri hao ni January Makamba (Muungano na Mazingira ), Dk Charles Tizeba (Kilimo na Mifugo na Uvuvi), Dk Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Mwigulu Nchemba (Mambo ya Ndani ya Nchi). Wengine ni Profesa Jumanne Maghembe (Maliasili na Utalii) na Seleman Jafo (Naibu Waziri wa Tamisemi) wakati Wizara ya Uchukuzi iliwakilishwa na katibu mkuu, Dk Leonard Chamulilo. 

Akizungumza na wanahabari jana baada ya kikao hicho, Makamba alisema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadiliana namna ya kuchukua hatua za kukabiliana na uvuvi huo. 

Makamba ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali za bahari na samaki, lakini zinaathiriwa na uvuvi haramu. 

“Tumejadiliana kwa kirefu na tumetafakari hatua za kuchukua ili kukomesha tabia hii. Kikao kilikuwa cha kazi, mikakati na mbinu za kukabiliana na watu wanaofanya uvuvi haramu,” alisema Makamba. 

Hata hivyo, hakuwa tayari kuzitaja hatua walizokubaliana na mawaziri wenzake badala yake alisema taarifa kwa kina itatolewa siku zijazo. 

Kwa mujibu wa Makamba, baada ya miezi sita mawaziri hao watakutana na kupeana mrejesho wa kujua hatua walizokubaliana zimefanikiwa kwa kiwango gani. 

“Shughuli hii ni vita, lazima tupambane. Nguvu ya Serikali iliyopo hapa (mawaziri) itawashukia wahusika pasipo kujua,” alisema Makamba. 


Dk Tizeba alisema mazingira ya bahari yanazidi kuharibika na kwamba asilimia 40 ya matumbawe ya samaki yameathiriwa na uvuvi huo. 

“Lazima tuchukue hatua madhubuti kukomesha uvuvi haramu. Tumejipangia hatua za muda mrefu na mfupi katika hili,” alisema. 

Waziri huyo aliongeza kuwa Tanzania ndiyo nchi iliyobaki na aibu ya kuvua samaki kwa kutumia milipuko ya mabomu, jambo linaloiletea sifa mbaya. 

Nchemba alieleza kuwa kila Mtanzania ana wajibu wa kushirikiana na Serikali kukomesha vitendo hivyo kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola. 

“Wafichueni wote wanaofanya vitendo hivi na motisha ipo kwa mtoa taarifa,” alisema Nchemba.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages