Zitto Kabwe Aitaka Serikali Itangaze Balaa la Njaa

Zitto Kabwe Aitaka Serikali Itangaze Balaa la Njaa

Kiongozi wa Chama cha ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali kutangaza rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria kutokana na hali ya chakula kuwa mbaya nchini.

Kauli ya Zitto imetolewa wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisisitiza utunzaji wa chakula baada ya kukagua maghala ya nafaka yanayomilikiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kanda ya Songea.

Agizo la Majaliwa pia limetolewa siku mbili baada ya Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kutofautiana na Zitto kuhusu hali ya chakula ambapo Waziri huyo alisema hali ya chakula nchini ni shwari huku Mbunge huyo wa Kigoma Mjini akisema ni mbaya.

Jana, mbunge huyo akihutubia mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Kata ya Nkome, Geita aliendelea kupigilia msumari kauli yake akisema, “Hali ya chakula ni mbaya, ni mbaya, ni mbaya.”

Alisema baada ya ziara ya Waziri Mkuu kwenye maghala ya Taifa na kujionea hali ya chakula nchini, ni vyema Serikali ikachukua hatua.

“Ninapendekeza Serikali ichukue hatua muhimu ya kisheria ya kutangaza baa la njaa nchini. Tamko la baa la njaa litaisaidia Serikali kupata bajeti ya dharura ya kununua chakula na kutoa uhuru kwa wakuu wa wilaya kutangaza bila woga kuwa maeneo yao yana njaa,”alisema Zitto huku akimpongeza Majaliwa kwa ziara hiyo.

Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages