Saida Karoli Asimulia Alivyoporwa Haki Zake Katika Muziki Kisa Kutojua Kusoma na Kuandika

Saida Karoli Asimulia Alivyoporwa Haki Zake Katika Muziki Kisa Kutojua Kusoma na Kuandika

Jana kupitia kipindi cha Take One  cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi  alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili  Saida Karoli ambapo alikiri kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo.

Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia  ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea.

”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure

”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja

“Meneja wa zamani aliniuliza nyimbo yako inatakiwa kutumika lakini nipe idhini yako japo ni nyimbo zangu zote lakini sikuwa na haki licha ya kuwa sauti yangu imesikika kule, mimi nilimjibu nimeshakata tamaa na kuimba naona muziki kwangu hauna faida na thamani bora kuwa hata mkaanga vitumbua au maandazi kuliko kuimba

”Nilikuwa na mpango wa kurudi kijijini nyumbani nikae mtu akihitaji show atanikuta kijijini lakini meneja akanambia hapana, alisema nyimbo tumpe Diamond kwa sababu itaniinua na kunipa moyo na kuniamsha upya kama mtu aliyekufa

“Walizushaga nimekufa na nilihisigi nimekufa kweli kutokana na hali ya maisha na nilikuwa nimekata tamaa nikajua nimekufa kweli” AlisemaSaida Karoli

Kwa sasa Saida yupo Dar na amekuja rasmi kwa ajili ya kufanya muziki upya kama zamani na yupo tayari kufanya kolabo na wasanii kama Ben pol, Bell 9, Diamond na Darassa.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages